"Mungu wangu! Huyu si ndugu wangu Mwaliko?" Umu alisema kimyakimya. Dick naye alikuwa kaghumiwa, hajui la kusema. Anamtazama mnuna wae kana kwamba ni Mr Super Man katika sinema pendwa za kijasiri. Wote wawili walitazamana, kila mmoja akiapa moyoni kuwa amewahi kumwona kiumbe huyu mahali, lakini hakuna aliyedhubutu kunena ...
Tamaa ya kumiliki nyenzo za kujiinua kiuchumi na kisiasa, kama inavyodhihirika katika riwaya hii, inasambaratisha asasi za kijamii, pamoja na miundomsingi ya mshikamano wa kijamii. Maazimio yasiyofikiwa yanazua hali ya kuunjikiwa - kihoro hasa. Lakini baada ya kiza kizito huja mawio ya uzawa wa jamii mpya yenye matumaini.
Assumpta K. Matei ni mtafiti na mwalimu mwenye tajiriba pana katika ufundishaji wa lugha na fasihi ya Kiswahili katika shule za upili na vyuo vikuu. Kati ya taaasisi alizowahi kufundisha ni Kenya High School na Catholic University of Eastern Africa. Ameshiriki katika majopo mbalimbali ya ukuzaji, utekelezaji na tathmini ya mitaala.